Loading...

- Programu ya elimu ya lazima inalenga umma wa Kiislamu kwa ujumla na ina kozi maalumu zinazohusiana na maarifa ya lazima katika Dini na mambo ya msingi ya Dini. Masomo hayo yapo wazi muda wote wala hayana wakati maalumu.

Programu maalum ni programu ya kielimu inayojumuisha viwango na hatua kadhaa za masomo. Inalenga kutoa mwanafunzi ambaye ana ujuzi katika elimu ya Sharia na fani zake. Masomo yake yamewekewa muda maalumu, pia kuna mikutano ya moja kwa moja na walimu, dirisha la majadiliano, shughuli, baadhi ya kazi, na utaratibu sahihi wa mitihani. Mwanafunzi lazima afuatilie masomo na kuwasilisha kazi zinazohitajika kulingana na ratiba iliyoandaliwa.