Mpango huu unawalenga Waislamu kwa ujumla wanaotaka kujipatia elimu ya kisharia ya wajibu, na yale yanayojulikana wazi katika dini kwa msururu wa masomo yenye sanad ulioungana. Mpango huu unajumuisha idadi ya masomo yanayowasilishwa kwa mbinu za kielimu zilizo thabiti na kwa njia iliyorahisishwa, Masomo yake yako wazi bila kuwekewa muda maalumu; hivyo mwanafunzi anaweza kujisajili, kusoma masomo, na kuyakamilisha kwa wakati na muda anaoona unamfaa.