Programu ya kielimu yenye isnadi kwa mujibu wa mbinu ya kielimu iliyodhibitiwa, inajumuisha idadi ya viwango na hatua za masomo, inalenga kutoa mwanafunzi aliyebobea katika elimu za Sharia na Fani zake, na hii ni maalumu kwa mwenye juhudi na uwezo wa kujitolea katika nyakati zilizopangwa, kwa sababu masomo yamewekewa muda maalumu kulingana na ratiba ya masomo kwa kila somo (Kozi), na masomo yake yanajumuisha mikutano ya moja kwa moja na walimu na nafasi ya majadiliano, na shughuli na baadhi ya kazi za nyumbani na utaratibu makini katika mitihani, na ni lazima kwa mwanafunzi kufuatilia masomo na kuwasilisha kazi zinazotakiwa kulingana na ratiba iliyoandaliwa.